Majlisi hii imeandaliwa na kuratibiwa na Madrasat ya Mabinti ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni, Jijini Dar-es-salaam. Hii inaonyesha umuhimu wa pekee wa Wanawake wa Kiislamu katika kuandaa na kushiriki kwenye shughuli za kidini na kitamaduni.

27 Juni 2025 - 15:21

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Programu ya kihistoria imefanyika leo hii tarehe 27 Juni, 2025, kwa heshima na Utukufu wa Mwezi wa Muharram katika kumuenzi Imam Hussein (A.S) na Harakati yake ya Mapinduzi ya kihistoria ya Kiislamu aliyoyafanya katika Ardhi ya Karbala.

Majlisi ya Muharram - Madrasat Hazrat Zaynab (SA): "Muslim bin Aqil (RA) na mchango wake muhimu katika historia ya Uislamu" + Picha

Programu ya Majlis hii iliongozwa na: Sheikh Ghawthi katika Hawzat ya Mabanati ya Hazrat Zaynab (sa) - Iliyopo Kigamboni, Dar-es-salaam. 

Majlisi ya Muharram - Madrasat Hazrat Zaynab (SA): "Muslim bin Aqil (RA) na mchango wake muhimu katika historia ya Uislamu" + Picha

Mada kuu ya khutba yake ilikuwa ni kuhusiana na: 

"Muslim bin Aqil (RA) na mchango wake muhimu katika historia ya Uislamu".

Aidha, tukio hili kama ilivyodokezwa hapo juu liliandaliwa na kufanywa na Madrasat ya Mabinti ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni, Dar-es-salaam. 

Hii inaonyesha umuhimu wa pekee wa wanawake wa Kiislamu katika kuandaa na kushiriki kwenye shughuli za kidini na kitamaduni. 

Majlisi ya Muharram - Madrasat Hazrat Zaynab (SA): "Muslim bin Aqil (RA) na mchango wake muhimu katika historia ya Uislamu" + Picha

Muslim bin Aqil (RA), ambaye alikuwa mjumbe wa Imam Hussein (A.S) katika mji wa Al-Kufa, ni shujaa muhimu katika historia ya Karbala na Mapinduzi ya A'shura. 

Kumbukumbu ya ujasiri na dhabihu zake katika kipindi hiki cha Muharram ni muhimu sana kudurusiwa na kuhadithiwa, Kwani zimebeba masomo matukufu ndani yake kwa Umma wa Kiislamu.

Programu kama hizi, mbali na kumuenzi Imam Hussein (A.S) na tukio la A'shura, pia husaidia kuimarisha utambulisho wa kidini na kitamaduni miongoni mwa Waislamu. 

Majlisi ya Muharram - Madrasat Hazrat Zaynab (SA): "Muslim bin Aqil (RA) na mchango wake muhimu katika historia ya Uislamu" + Picha

Aidha, zinaweza pia kuwa chombo cha kuelimisha vijana kuhusu mafunzo ya A'shura, kama vile kujitoa, kujitolea, na kupigania haki, hata katika hali ya maumivu na mateso makubwa, hutakiwi mtu kuwa upande wa batili, bali daima dawamu unatakiwa kuipenda Haki na kuwa tayari kuitetea na kuihuisha.

Majlisi ya Muharram - Madrasat Hazrat Zaynab (SA): "Muslim bin Aqil (RA) na mchango wake muhimu katika historia ya Uislamu" + Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha